Je wajua kwamba kemikali unazotumia kila siku zinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwa watoto na familia? Je wajua kwamba viuatilifu vinavyotumika mashambani ni sumu na vinaweza kusababisha madhara makubwa kwenye mwili wa mwanamke? Kozi hii ya sayansi na afya ni moja wapo ya suluhisho. Tunakushauri ufuate kozi hii hadi mwisho, halafu uchukue hatua.   

This course is presented in Swahili, with English subtitles. A version of this course with materials and quizzes in English can be found in our course catalog.


Dk. Aiwerasia Vera Festo Ngowi

Ana shahada ya Uzamivu katika Epidemiolojia, Chuo Kikuu cha Tampere, Finland; Stashahada katika Afya na Usalama Kazini kivitendo; Taasisi ya Kitaifa ya Maisha ya Kufanya Kazi, Stockholm, Sweden; Shahada ya Uzamili ya Sayansi za Afya Kazini; Chuo Kikuu cha Manchester, Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini; Stashahada katika Sayansi na Teknolojia ya Mazingira, Delft, Uholanzi; Shahada ya kwanza ya Kemia na Sayansi ya Muundo wa Mimea, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam, Tanzania.

Kwa sasa ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Afya Mazingira na Kazini katika Skuli ya Sayansi za Afya ya Umma na Jamii, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar-es-Salaam, Tanzania. Anafundisha na Kusimamia tafiti za wanafunzi wa Chuo Kikuu wa shahada ya kwanza, Uzamivu na Uzamili katika nyanja za kemikali (hasa viuatilifu) na afya. Alikuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi zisizo za kiserikali za Programu ya Afrika ya Kuondoa Mlundikano wa Viuatilifu Chakavu (ASP (T) Network) na Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Wataalam wa Afya ya Umma, Kazini na Mazingira (TAPOHE).

Dkt. Dorothy Ngajilo ni Daktari Bingwa wa magonjwa yanayosababishwa na kazi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MoHCDEC), Tanzania. Ana shahada ya udaktari (MD) kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Tanzania, na Shahada ya Uzamili ya Tiba (MMed) katika tiba ya magonjwa yanayosababishwa na kazi, kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town (UCT), Afrika Kusini. Pia ni mbobezi wa masuala ya sayansi ya tiba ya magonjwa yanatosababishwa na kazi (FCPHM (SA) Occ Med), kutoka “College of Medicine of South Africa (CMSA)”. Amejikita kwenye utafiti wa kutathmini na kudhibiti migusano hatarishi inayotokana na kazi pamoja na mazingira, hasa kwa wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi na wanawake.

Ms. Baldwina Tita Olirk 

Miss Baldwina Tita Olirk ni mtaalam wa Afya ya Mazingira na mahala pa kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Yeye pia ni mhadhiri wa heshima katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Ana Shahada ya kwanza katika Sayansi ya Mazingira na Usimamizi na Shahada ya Uzamili katika Afya ya Mazingira na mahala pa kazi iliyofunzwa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Masilahi yake ya utafiti ni mgusano wa viuatilifu na uhusiano wake na athari za kiafya za muda mrefu miongoni mwa wanawake wanaofanya kazi za kilimo.

Choose a Pricing Option

This course "Science and Health" is part of IPEN's Women and Chemicals training series. The course is presented in Kiswahili (with English subtitles) by Aiwerasia Vera Ngowi And Team from Tanzania Association of Public, Occupational and Environmental Health Experts (TAPHOE) in Tanzania


This material has been produced with the financial contribution by the Swedish International Development Cooperation Agency (Sida) through the Swedish Society for Nature Conservation (SSNC). The views herein shall not necessarily be taken to reflect the official opinion of SSNC or its donors.